Friday, October 21, 2011

FROM TCU

                                                 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania

                                                     TAARIFA KWA UMMA

 Tume  ya  Vyuo  Vikuu  Tanzania  inautaarifu  umma  kuwa  utaratibu  wa 
kuomba  udahili  kwa  vyuo  vya  elimu  ya  juu  ambavyo  bado  vina  nafasi 
unaandaliwa na kwa mantiki hiyo wale wote ambao hawana udahili kwa 
sasa  na wangependa  kuomba  kujiunga  na  vyuo  hivyo  katika mwaka wa 
masomo    2011/12  wasubiri  mpaka  utaratibu  huo  utakapotangazwa  na 
Tume kuanzia tarehe 26 Septemba 2011. 


Matangazo  ambayo  yametolewa  na  Chuo  Kikuu  cha  Dar  es  salaam
kuitisha  udahili  zaidi  kwa  sababu  ya  chuo  hicho  kuwa  na  nafasi  katika
programu mbalimbali ni ishara kwamba bado kuna nafasi katika programu
za chuo hicho na hivyo wanafunzi wasubiri utaratibu wa kuomba udahili
katika vyuo utakapotangazwa na Tume kuanzia tarehe 26 Septemba 2011
ili kuepuka usumbufu wanaoweza kuupata hapo baadaye.


Kwa  taarifa  hii vyuo  vikuu  vyote  nchini  vinataarifiwa  kusubiri utaratibu
utakapotangazwa  kabla  ya  kutoa  matangazo  yao.  Pia  vyuo  vyote  vya
elimu  ya  juu  ambavyo  bado  vina  nafasi  kwa  ajili  ya  wanafunzi  kwa
mwaka  wa masomo  wa  2011/12  vinataarifiwa  kutuma  taarifa  hizo  kwa
Tume  ili  programu  husika  ziweze  kuongezwa  kwenye mfumo  kabla  ya
tarehe 26 Septemba 2011.
Heri ya miaka 50 ya Uhuru

                           Katibu Mtendaji
       TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA

No comments:

Post a Comment